Kampeni ya Usafi sasa ni Mkoa kwa Mkoa

0
131

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita kuwa sehemu ya mfano kwa kuzingatia usafi katika mazingira yanayowazunguka kwa hiari.

Waziri Bashungwa ametoa wito huo wakati akizindua wa Kampeni ya usafi wa mazingira Mkoa wa Geita na kauli mbiu ya “Mwanamke ni chachu ya usafi wa mazingira; Tuungane katika kutunza mji wetu”

“Utaratibu mliouweka kila wiki kufanya usafi mshirikiane na makapuni yanayochimba dhahabu hapa Geita na wadau wengine kuhakikisha tunakuwa na Geita safi inayomelemeta” amesema Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Geita kushirikiana na Baraza la madiwani kuweka mikakati ya kuboresha stendi ya mkoa huo ili kuwa na stendi bora na ya kisasa inayoutambulisha Mkoa wa Geita.