Kamati za Bunge zaitwa Dodoma

0
276

Kufuatia kifo cha Rais John Magufuli, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, ameziagiza kamati zote za Bunge zilizokuwa katika ziara za kukagua miradi ya maendeleo mikoani kurejea jijini Dodoma mara moja.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Spika jijini Dodoma imeeleza kuwa, Spika Job Ndugai amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha Rais  Dkt Magufuli ambaye alijitoa kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu.

Rais Magufuli amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es salaam akiwa na umri wa miaka 61.