Kamati ya Mawaziri yatumia Bodaboda kuwafikia wananchi

0
130

Utatuzi wa migogoro ya Ardhi mkoani Tabora umechukua sura mpya baada ya kamati ya mawaziri nane kulazimika kupanda bodaboda ili kuwahi kufika katika maeneo ya wananchi.

Katika wilaya ya Uyui Tabora kaskazini vijiji 12 vyenye wakazi zaidi ya elfu moja vimepata neema ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kubaki katika maeneo yao na kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Takribani mikoa minne imeshatoa mrejesho wa maamuzi ya baraza la mawaziri chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Idadi kubwa ya vijiji vilivyovamia hifadhi vimetaka kubaki katika maeneo yao.