Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na corona kuimarishwa

0
169


Serikali imeamua kuimarisha Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na virusi vya corona, ambayo kwa sasa itakuwa chini ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaidiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Hayo yameelezwa na Rais John Magufuli wakati akihutubia Taifa kuwaeleza Watanzania kuhusu virusi hivyo ya corona, ambapo mpaka sasa wagonjwa kumi na wawili nchini wamethibitika kuugua ugonjwa huo.
Amesema Wajumbe wengine wa Kamati hiyo watachaguliwa na kutangazwa na Waziri Mkuu Majaliwa kulingana na umuhimu wao.
K

Katika hotuba yake, Rais Magufuli ameipongeza wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, vyombo vya habari nchini pamoja na watu mbalimbali walioshirikiana na serikali katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu virusi hivyo vya corona.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za Shirika la Afya Duniani (WHO) zaidi ya watu laki mbili na sitini kwenye nchi takribani mia moja na sitini duniani wameambukizwa virusi vya corona, huku waliofariki dunia wakifikia zaidi ya elfu 11.