Kamati ya Bunge ya Miundombinu yafanya ziara TBC

0
137

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu leo imefanya ziara katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo mkoani Dar es Salaam.

Katika Makao Makuu ya TBC, barabara ya Nyerere wajumbe wa kamati hiyo wamejionea ukarabati mkubwa wa studio za redio za TBC Taifa na TBC FM pamoja na studio za kidigitali za makumbusho ya Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Wamejionea pia utendaji kazi katika vitengo mbalimbali na kupata maelezo ya namna kazi zinavyofanyika.

Wakiwa barabara ya Nyerere wajumbe wa kamati hiyo ya Kudumu ya Miundombinu wametembelea eneo la TBC lililovamiwa na wafanyabiashara wadogo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania DKt. Ayub Rioba Chacha amewaeleza wajumbe hao kuwa kuwa utaratibu wa kuwaondoa wafanyabiashara hao wadogo unafanyika ili kulilinda eneo hilo.