Waziri mpya wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuendelea kumuamini na kumpatia nafasi hiyo.
Profesa Kabudi ametoa shukrani hizo wakati wa hafla ya kuapishwa kwa viongozi mbalimbali, hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.
Profesa Kabudi amemuahidi Rais Magufuli na Watanzania wote kuwa atatekeleza majukumu yake kikamilifu.
Akitoa salamu zake baada kula kiapo, Profesa Kabudi amewaagiza viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufanya mabadiliko ya kiuendaji ndani ya wizara hiyo wakianzia na wao wenyewe.
Katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Magufuli Machi Tatu mwaka huu, Profesa Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoka wizara ya Katiba na Sheria.
Balozi Augustine Mahiga aliyekua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amehamia wizara ya Katiba na Sheria.