JPM akoshwa na Jeshi la Polisi, aahidi bilioni 1.5

0
238

Rais Dkt. John Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa IGP Simon Sirro kwa kazi nzuri wanayofanya hasa katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo, Temeke mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya ufunguzi wa majengo ya ofisi na madarasa pamoja na bweni la wanafunzi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi.

Kutokana na kufurahishwa na juhudi za chombo hicho cha ulinzi kwa kujenga mabweni, madarasa na kiwanda cha ushonaji wa sare za polisi, Rais Magufuli ameahidi kutoa shilingi bilioni 1.5 ambapo bilioni 1 ni kwa ajili ya kujenga mabweni mawili na kiasi kilichobaki kwa ajili ya ujenzi wa hospitali.

Amelipongeza jeshi la polisi kwa namna linavyoendelea kulinda raia na mali zao ambapo taarifa iliyotolewa na IGP Sirro imeeleza kuhusu kupungua kwa matukio mbalimbali ikiwamo ajali za barabarani na wizi wa kutumia silaha.

amelipongeza Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa IGP Simon Sirro kwa kazi nzuri wanayofanya hasa katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia.