Joyce Shebe: Wanahabari tuzingatie weledi kwenye kazi

0
223

Mhariri Mkuu wa Clouds Media Group, Joyce Shebe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania-TAMWA amesema mwaka 2022 ni muhimu waandishi wa habari kusimamia weledi na majukumu yao katika kazi ya uandishi wa habari kwa manufaa ya watanzania na Taifa kwa ujumla

Shebe ameyasema hayo wakati akiwa katika kipindi cha Jambo Wikiendi kinachorushwa na Televisheni ya Taifa – TBC1

“Kwenye uandishi tuna majukumu ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha lakini unaandika ili iweje ‘so what’ bado jukumu letu lipo palepale tumeingia mwaka mpya bado Watanzania wanahitaji kusikia kutoka kwenye vyombo vya habari vinavyoaminika”

Aidha Shebe amesisitiza umuhimu wa taarifa za ukweli kwa Watanzania
“Wanahabari wabebe dhamana ya taarifa zinazoaminika maana ukweli ndo kila kitu katika taarifa yoyote mwandishi wa habari atakayo andika iwe ya kweli” amesema Joyce Shebe