JOB NDUGAI: UKIJIFANYA MBUNGE BUBU BUNGENI, UMEUMIA

0
262

Spika mteule wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewataka wabunge waliochaguliwa na wananchi kutokaa kimya ndani ya Bunge kwani wananchi wamewachagua kwa ajili ya kuwasemea changamoto na kutafutiwa ufumbuzi.

Akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge, Ndugai amesema, wabunge wanapaswa kujua walichokifuata ndani ya Bunge na kukaa kimya sio nidhamu bali ni kutowandekea haki wananchi waliowachagua.

“Waheshimiwa wabunge msidhani kukaa kimya ndani ya bunge ndio utaonekana una nidhamu, mko hapa kwa niaba ya wananchi, wasemeeni matatizo yao kwa uwazi”.-Amesema Job Ndugai.

Aidha Ndugai amewaomba waandishi wa habari kuandika na kusambaza taarifa zote za bunge kwa wananchi ili wafahamu mambo yanayojadiliwa.

“Ndugu zetu waandishi wa habari lazima Bunge hili lionekane, lisikike kwa hiyo ni jukumu lenu kuhabarisha umma habari za bunge”-Amesema Job Ndugai

Katika hatua nyingine wabunge walioteuliwa, wameapa kiapo cha uaminifu kulitumikia bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.