Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda mafunzo ya kujitolea ya JKT kwa mwaka 2020/2021 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni kwenye kambi mbalimbali nchini.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JKT imeeleza kuwa mafunzo hayo yamesitishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Kutokana na kusitishwa huko, JKT imewataka vijana wote ambao walichaguliwa na tayari wameripoti kwenye kambi walizopangwa, kurejea majumbani mwao.
Aidha, wale ambao walikuwa bado hawajaripoti kambini, wametakiwa kutoripoti.