Jeshi la Zimamoto lasisitiza kutolewa kwa elimu ya uokoaji

0
428

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Tanzania limesema, limekua likitoa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto pamoja na kuanzisha klabu za masuala hayo katika shule mbalimbali ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kukabiliana na ajali za moto.

Akizungumza na TBC, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Elia Kakwembe amesema licha ya jitihada hizo, bado elimu ya kukabiliana na majanga ya moto ni mdogo miongoni mwa Watanzania, na kwamba jitihada zaidi zinahitajika.

Kauli hiyo imekuja ikiwa Tanzania inaomboleza vifo vya wanafunzi 10 wa Shule ya Msingi Islamic Byamungu mkoani Kagera vilivyosababishwa na moto ulioteketeza bweni la wavulana.

Aidha, wanafunzi wanne kati ya sita waliokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali teule ya Wilaya ya Karagwe mkoani humo wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa, Bugando, jijini Mwanza kwa ajili kupatiwa matibabu zaidi.