Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Yusuph Masauni amesema Jeshi la Polisi halitayumbishwa katika kuhakikisha wanalinda usalama na kutoa onyo kwa wote wenye kupanga njama za kuvuruga nchi kuacha mara moja.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwatunuku vyeti askari waliofanya vizuri katika mafunzo ya uafisa na ukaguzi wa jeshi la polisi Masauni amesema serikali imejipanga kuhakikisha usalama wa nchi uko vizuri kwa gharama yeyote.
Naibu Waziri Masauni amewasisitiza wahitimu kuendeleza uzalendo na nidhamu kama mafunzo aliyoyapata na kwamba atashangaa endapo watakiuka yote waliyofunzwa.
Amewataka askari hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kufuata taratibu zinazotakiwa.