Jenista: Mafunzo ya Uanagezi ni muhimu kwa Vijana

0
143

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na wenye ulemavu amesema mfumo wa utoaji elimu za stadi mbalimbali za kazi unafanywa na serikali unalenga katika kutua ujuzi kwa vijana na kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

Akitoa maelezo ya mafunzo ya awamu ya tatu ya Uanagezi yanayotolewa na vyuo zaidi ya 70 nchi nzima Waziri Jenista amesema, mafunzo hayo yanawawezesha vijana kuwa na ujuzi na kuwa na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa.

Mhagama amesema, mafunzo hayo yamepitishwa na maabara ya kimataifa ya ajira hivyo yana hadhi ya kimataifa na vijana wote wanaopatiwa mafunzo hayo watakuwa na uwezo mkubwa na kutumia stadi zao katika kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo amesema, awamu ya kwanza na awamu ya pili ya mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwani vijana wengi wameweza kujiajiri na wengine kuanzisha karakana zao za kutoa huduma.

Mafunzo ya awamu ya tatu ya uanagezi yamezinduliwa hii leo Agosti 2, 2021 ambapo zaidi ya vijana elfu kumi na nne wanashiriki mafunzo ya waka huu na wanapatiwa stadi mbalimbali za kuwawezesha kujiajiri wenyewe baada ya mafunzo hayo.