Jengo la kihistoria la Bait-Al Jaib laporomoka

0
285

Jengo la kihistoria la Bait-Al Jaib lililoko eneo la Forodhani Visiwani Zanzibar, ambalo linajulikana sana kama nyumba ya maajabu limeporomoka wakati likiendelea kufanyiwa ukarabati.

Habari za hivi karibuni kutoka Zanzibar zinaeleza kuwa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi anafanya ziara katika eneo la tukio hilo ili kujionea madhara yaliyotokea.

Jengo hilo la kihistoria la Bait-Al Jaib ni miongoni mwa majengo ya urithi wa dunia yanayotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).