Jamii yakumbushwa kutumia taarifa sahihi kwenye majanga

0
291

Jamii imetakiwa kutumia njia sahihi za upatikanaji wa taarifa kuhusu masuala ya Afya ili kuepuka kupotoshwa na vyanzo vya taarifa visivyo sahihi na kupelekea taharuki kutokana na janga husiki linalotokea

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Shirika la PHEDES Tanzania John Ambrose ambaye pia ni mkufunzi wa masuala ya Afya ya Akili na msaada wa Kisaikolojia ambapo Kupitia Shirika hilo na Amref wanaendale na mafunzo kwa maafisa ustawi wa Jamii, wahudumu wa Afya na azaki zianazotoa huduma za Afya ya Jamii Mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa huduma bora kwa jamii.

Padri Thresphory Tweve wa Jimbo la Katoliki la Mbeya na mratibu wa shughuli za VVU na Ukimwi Jimbo amesema kwa nafasi yao kama viongozi wa Dini wananafasi kubwa ya kusikilzwa na waumini wao hivyo kuwaomba viongozi wenzake kutoa taarifa sahihi kutoka mamlaka za Serikali na viongozi Wakuu wa Dini zao ili Kurahisisha kutoa elimu ya majanga yanapotokea kwenye Jamii

Kwa upande wake Daktari wa Afya ya Akili Hospitali ya Mkoa Mbeya Dkt. Reinfridy Chombo amesema mtu yeyote anapoenda kununua dawa kwaajili ya matibabu maduka ya dawa anapaswa kujirishisha kupata taarifa sahihi ya dawa yenyewe ili kuepukana na madhara ya dawa yanayoweza kusababishwa na matumizi mabaya ya tawa husika.

Aidha Deborah Dikoko Mratibu wa Afya ya Akili Mkoa wa Mbeya ameeleza kuwa wamekuwa wakipokea wagonjwa walioathilika taarifa zisizosahihi na kuwapelekea kuwa na matatizo ya Afya ya Akili ikiwepo kupuuza maelekezo ya kitaalam hasa wakati wa uzazi na malezi.