Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wafanyakazi kuwa ahadi ya kuwaongezea Mshahara aliyoitoa mwaka jana wakati wa sherehe za Mei Mosi jijini Mwanza ipo pale pale.
Akihutubia wakati wa sherehe za mwaka huu za siku ya wafanyakazi Duniani zinazofanyika Mkoani Dodoma, Rais Samia amesema “lile jambo letu lipo ila sio kama lilivyosemwa na TUCTA” akimaanisha utekelezaji wa ahadi hiyo upo pale pale