Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania afariki dunia

0
533

Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kati ya mwaka 2006 hadi 2010, Augustino Ramadhani amefariki dunia, mahakama nchini Tanzania imeeleza.

Jaji Ramadhani amefikwa na umauti leo Aprili 28, 2020 katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumzia hilo matoto wa marehemu, Yakud Ramadhani amesema baba yake aliuguwa kwa muda mrefu na pia amewahi kwenda kutibiwa nchini Kenya.

Yakud amesema kwa sasa familia inaendelea na taratibu nyingie, na kwamba umma utajulishwa kitakachofuata.

Kiongozi huyo alizaliwa visiwani Zanzibar na katika kipindi cha uhai wake miongoni wa nyadhifa ambazo ameshika ni pamoja na kuwa
Jaji Mkuu wa Zanzibar.

Nyadhifa nyingine ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.