Jaji Mkuu asisitiza usuluhishi ndani ya jamii

0
192

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesisitiza suala la usuluhishi na upatanishi miongoni mwa pande zenye migogoro.

Jaji Mkuu ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa jengo la mahakama ya mwanzo ya Kibaigwa.

Amesema si lazima kila shauri kwenda mahakamani, na badala yake pande zinazopingana zinaweza kusuluhushwa na kupatanishwa.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, hatua hiyo itasaidia kupunguza mashauri mahakamani na kuziwezesha pande zenye migogoro kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Amesema kuna sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu usuluhishi, hivyo ni vema sheria hiyo ikafahamika na kutumika miongoni mwa jamii.

Ujenzi wa jengo hilo la mahakama ya mwanzo ya Kibaigwa umegharimu shilingi milioni 797 hadi kukamilika kwake.