Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mkusa Issack Sepetu, amefariki dunia asubuhi leo Februari 16, 2020 mjini Unguja.
Afisa Habari wa Mahakama Kuu Zanzibar ameeleza kuhusu kifo hicho katika taarifa kwa umma aliyoitoa muda mfupi uliopita.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa maziko yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni kijijini kwao Mbuzini, wilayani Magharibi A, Unguja.
Enzi za uhai wake Jaji Sepetu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na baadae Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar.