IGP Sirro awaonya wanasiasa wanaotumia vibaya mitandao

0
190

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewataka wanasiasa nchini kutumia vizuri mitandao ya kijamii hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo mkoani Manyara wakati akizindua jengo la kituo cha polisi katika kijiji cha Yaeda Chini wilayani Mbulu.

Amesema ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa za kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii katika kuwachonganisha wananchi na serikali yao.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini amesisitiza kuwa jeshi hilo liko imara katika kukabiliana na mtu yeyote atakayevunja sheria za nchi, na kuwataka wanasiasa kote nchini kutotenda makosa na kujificha kwenye mwamvuli wa siasa.