IGP Sirro awahamisha makamanda wawili wa polisi

0
461

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo ya kuwahamisha baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi za Polisi.

Sirro amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Revocatus Malimi kutoka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Juma Haji.

Pia amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Omary Said Nassiri kutoka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi.