IGP Sirro, asisitiza viongozi kulinda amani

0
374

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka viongozi wa siasa, tume na wadau wengine wa siasa kutimiza wajibu wao katika kulinda amani ya nchi wakati huu wa uchaguzi.

“Tunatarajia kumpata rais mmoja atakayechaguliwa na wananchi hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake kudumisha amani iliyopo.”- Amesema IGP Simon Siro.

Ameongeza kuwa jeshi la Polisi limejiandaa kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa huku akiwasisitiza wapiga kura, kwenda kupiga kura bila woga nakuepuka vurugu katika vituo vya kupigia kura.