IGP Sirro ajitambulisha kwa Dkt. Mwinyi

0
221

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro Ikulu jijini Zanzibar.

IGP Sirro alikwenda kujitambulisha rasmi kwa Rais Dkt. Mwinyi.

Wakati wa mazungumzo hayo, Dkt. Mwinyi amelipongeza Jeshi la Polisi Nchini kwa kazi nzuri linalofanya na kulitaka kuendelea kufanya kazi hiyo nzuri ya kulinda Raia na mali zao.