IGP Sirro aagiza operesheni kudhibiti makosa barabarni

0
232

Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Simon Sirro amewaagiza Makamanda wa polisi nchini kufanya operesheni ya mwezi mmoja ya kudhibiti makosa ya barabarani ambayo kwa kipindi cha mwezi huu yameongezeka.

IGP Sirro ametoa agizo hilo mkoani Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Rufiji pamoja na wakuu wa vikosi vya usalama barabara wa mikoa na wilaya na wakuu wa pperesheni kutoka kwenye mikoa hiyo.

Kwa upande wa Wananchi, IGP Sirro amewataka kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani, lengo likiwa ni kuepusha ajali zinazoweza kuepukia.