Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema idadi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Korogwe mkoani humo imefikia 20, baada ya majeruhi wawili waliokuwa wakipatiwa matibabu hospitalini kufariki dunia.
Mgumba ametoa kauli hiyo wakati wa ibada ya kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya hospitali ya wilaya ya Korogwe, Magunga.