Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa kitaalamu wa Benki ya Dunia wa tathmini ya utekelezaji wa mzunguko wa 20 wa mfuko wa IDA, utakaofanyika kwa muda wa siku tatu visiwani Zanzibar kuanzia Desemba 6 hadi 8, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil amesema tathmini ya mkutano huo itazingatia kufanya tathmini ya miradi inayotekelezwa katika nchi zenye kipato cha chini kupitia fedha za mkopo na msaada zinazotolewa na Mfuko huo uliopo chini ya Benki ya Dunia.
Katika hatua nyingine waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Saada Salum Mkuya wamempokea Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga ambaye amewasili visiwani humo kwa ajili ya kushiriki mkutano huo wa IDA.
Akiwa nchini Rais huyo wa Benki ya Dunia atapata fursa ya kufanya mazungumzo na
Rais Samia Suluhu Hassan na
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.
Mkutano huo wa IDA unatarajiwa kuwakutanisha wakopaji na wakopeshaji 75 , nchi wahisani 54 pamoja na viongozi wa Benki ya Dunia.