Ibada ya kuaga miili ya watoto wawili wa familia moja waliofariki dunia mkoani Mtwara baada ya breki za basi dogo la shule ya msingi ya King David kufeli na kutumbukia kwenye korongo inaendelea hivi sasa katika kanisa la Anglikana mkoani humo.
Watoto hao ni Johari Simon (7) na Emmanuel Simon (5, ambao baba yao ni mfanyakazi wa benki ya NMB mkoani Mtwara, Simon Jogwe.
Baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, miili ya watoto hao itasafirishwa kwenda Chamwino, Dodoma kwa ajili ya mazishi.
Katika ajali hiyo watu 13 walifariki duniani, 11 wakiwa ni wanafunzi wa shule hiyo ya msingi ya King David.