Hukumu kesi ya Membe yapigwa kalenda

0
119

Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe dhidi ya Mwandishi wa habari Cyprian Musiba imeahirishwa hadi tarehe 28 mwezi huu.
 
Hukumu hiyo ilikuwa itolewe hii leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam  na Jaji Joaquine De Mello, na  imeahirishwa kwa madai kuwa haijakamilika kuandikwa.
 
Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa madai ya kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.