Huduma za Kibingwa Zimeimarishwa

0
197

Takwimu za Wizara ya Afya zinaonesha kuwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, sekta ya afya imepata msukumo mkubwa ambapo miongoni mwa mengi yaliyofanyika ni pamoja na ununuzi na ufungaji wa vifaa tiba.

Upatikanaji wa mashine za kiuchunguzi katika ngazi ya vituo vya afya umerahisisha huduma kwa wananchi, umepunguza rufaa kwenda hospitali za juu pamoja na kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika.