Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema Serikali ya Mkoa wake umeanza juhudi ya kusambaza maji Safi na salama pembezoni mwa mji huo ili kuendelea kukabiliana na uhaba wa huduma ya maji kwa Wananchi wa maeneo hayo.
Akitoa salamu za mkoa kwenye Hafla ya kumkaribisha makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, Makalla amesema baada ya kupunguza kwa kiwango kikubwa changamoto ya maji Mjini sasa nguvu inaelekezwa nje ya mji
Aidha Makalla ameipongeza CCM kwa kuendelea kuisimamia Serikali katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho Katika kuwaletea maendeleo watanzania akitoa mfano wa uboreshaji wa miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo Ujenzi wa Barabara.