Hospitali ya rufaa Katavi kutoa huduma Januari

0
180

Muonekano wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92 na hadi kukamilika kwake ujenzi wake utakuwa umegharimu shilingi bilioni 12.4.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Katavi amekagua ujenzi wa hospitali hiyo na kumuagiza Mganga Mkuu wa hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Katavi Dkt. Patrice Serafin ahakikishe ifikapo Januari Mosi mwaka 2023 hospitali hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Pia amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Katavi kuhakikisha ifikapo tarehe 23 mwezi huu awe amefikisha huduma ya umeme katika hospitali hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospitali hiyo.