Naibu Waziri, Wizara ya Sheria na Katiba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu lililopo Mkoani Katavi, Geophrey Pinda ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel (@dorismollelfoundation), Doris Mollel katika kukabidhi mashine tatu za kufua hewa ya oxygen kwa ajili ya watoto njiti wanaozaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpimbwe, iliyopo mkoani Katavi.
Mgeni rasmi katika Makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Mlele Philbert Sanga amewaomba Segal Family Foundation @segalfoundation kuendelea kushirikiana na Doris Mollel Foundation ili waweze kurudi tena na kusaidia Hospitali mbalimbali Mkoani humo.
Naibu Waziri Pinda ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kuendelea kusaidia jamii ya Watanzania katika masuala ya uzazi na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kizalendo na kujitoa kusaidia jamii.