Hospitali ya bilioni 32 yafunguliwa Zanzibar

0
300
default

Rais Samia amefungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi (Lumumba), Zanzibar leo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itahudumia zaidi ya wananchi 800,000 umegharibu ya shilingi billioni 32.5 ambazo ni sehemu ya fedha za mkopo zilizopokelewa na Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na athari za UVIKO19.