Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Butiama, Jumanne Sagini ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel katika kukabidhi mashine tatu za kufua hewa ya oxygen kwa ajili ya watoto njiti wanaozaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama, iliyopo mkoani Mara.
Mgeni rasmi katika Makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Moses Kaegele ambaye amewaomba Segal Family Foundation kuendelea kushirikiana na Doris Mollel Foundation kupeleka vifaa hivyo kwenye maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi.
Naibu Waziri Sagini ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kuendelea kusaidia jamii ya Watanzania katika masuala ya uzazi na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kizalendo na kujitoa kusaidia jamii.