Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mosses Chitama akikata keki ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa ambayo pia ni siku yake ya kustaafu.
Katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya TBC, Chitama ametumia nafasi hiyo kuwaaga wafanyakazi wenzake na kuwasisitiza kudumisha umoja na ushirikiano, huku wakilitumikia kwa bidii na uzalendo shirika na Taifa kwa ujumla.