Historia ya gari lililobeba mwili wa Mkapa

0
302

Gari hili ndio lililobeba mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kuelekea uwanja wa Uhuru (Uhuru Stadium) kwa ajili ya viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.

Ni gari ya jeshi inayotumiwa na Amiri Jeshi Mkuu pekee na vilevile katika matukio makubwa ya nchi. Rais hutumia gari hii kuingia uwanjani siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania (Disemba 9).

Ikumbukwe kwamba mwaka 1999 gari hili lilibeba mwili wa Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.