Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema kazi ya kupambana na rushwa sio kwa taasisi pekee, bali ni wajibu wa kila Mwananchi kwani rushwa ni adui namba moja wa haki.
Abdulla amesema hayo jijini Arusha wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika, maadhimisho yanayojumuisha taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka mataifa zaidi ya 20 Barani Afrika.
“Ndugu zangu suala la kupambana na rushwa sio la TAKUKURU na ZAECA pekee bali hata sisi Wananchi tunao wajibu wa kuhakikisha tunapambana na rushwa kwa nguvu zote, na tukifanikiwa hapo naamini tutapiga hatua kubwa sana”.
Amesema
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Wakati wa maadhimisho hayo ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika yanayofanyika kwa muda wa siku ya tatu, kutakuwa na mijadala mbalimbali kuhusu namna bora ya kuzuia na kupambana na rushwa Barani Afrika.