Helikopta yatumika kusaka simba Iring

0
145

Serikali imetoa helikopta kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kuwasaka simba waliovamia vijiji kadhaa wilayani Iringa na kuua mifugo.

Helikopta hiyo imetua hii leo katika kijiji cha Tanangozi kilichopo wilayani Iringa na kuanza kuruka na wataalam wa shabaha wa wanyama pori wakifuatilia nyendo za simba hao.

Hadi kufikia leo asubuhi ng,ombe 23, nguruwe 10, kuku na mbuzi walikuwa wameuawa na simba hao ambao inasadikiwa wapo kwa makundi.