Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda ameiagiza wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inashughulikia changamoto za ndovu waliovamia makazi ya watu mkoani Lindi.
Chatanda ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Naipingo wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Amefafanua kuwa ndovu hao wamevamia makazi ya watu kutokana na Wananchi kuingia katika maeneo ya hifadhi.
Mwenyekiti huyo wa UWT Taifa ameelekeza hatua za haraka zichukuliwe kuwatoa Wananchi katika hifadhi ili kunusuru mazao yao yanayoliwa na ndovu pamoja na vifo vya Wananchi.
Kufuatia agizo hilo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja ameahidi wizara kupeleka helikopta kwa ajili ya kufukuza ndovu, ambayo itaweka kambi katika maeneo husika.
Amesema Serikali inajua Changamoto zinazowakabili Wananchi, hivyo imepanga kuongeza idadi ya askari na kujenga vituo vya askari ili kuondokana na tatizo la ndovu.