Hayati Dkt Magufuli atajwa kinara wa maboresho NECTA

0
190

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema litaendelea kumuenzi na kumkumbuka  aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, kwa jitihada zake za kulifanya Taifa kuondokana na utegemezi wa misaada kutoka mataifa mengine.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Charles Msonde na kuongeza kuwa wakati wa uongozi wake, Dkt Magufuli alilipatia Baraza hilo zaidi ya shilingi bilioni 12 ili liweze kununua mitambo ya kisasa ya TEHAMA.

Amesema.kabla ya kununuliwa kwa mitambo hiyo, baadhi ya shughuli za NECTA zililazimika kufanywa nje ya nchi, lakini baada ya Dkt Magufuli kutoa fedha na kununuliwa kwa mitambo hiyo ya kisasa, shughuli hizo zilianza kufanyika nchini.

Dkt Msonde amesema kutokana na mageuzi makubwa ya kiutendaji yaliyofanywa ndani ya NECTA wakati wa kipindi cha uongozi wa Hayati Dkt Maguguli, baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kutuma maombi katika Baraza hilo ya kutaka kwenda kufanya shughuli zao mbalimbali ikiwa ni.pamoja na kuchapisha mitihani.