HATUTOI KIBALI KWA GOBORE

0
219

Mkuu wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi nchini Reinada Millanzi amewataka wananchi kuzingatia sheria ikiwemo ile ya udhibiti wa silaha na risasi ya mwaka 2015 ambayo imekataza na kuzuia utoaji wa kibali cha silaha aina ya gobore.

“Kabla ya mwaka 2015 kurudi nyuma wananchi walikuwa wanaruhusiwa kumiliki magobore na yalikuwa yanawasaidia katika shughuli za ulinzi, lakini sasa kwa sheria hii ya mwaka 2015 imekataza.” amesema Millanzi

Ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania, ambapo hasa amezungumzia zoezi la usalimishaji wa silaha kwa hiari.

Pia Mkuu huyo wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi nchini amesema jeshi hilo linafahamu kuwa bado magobore yapo na yanendelea kukamatwa ambayo si halali, lakini wanomiliki kihalali wazingatie sheria.

“Sheria ya 2015 imekataza lakini wale waliokuwa wanamiliki gobore kihalali na walikuwa wanalipia katika halmashauri wale wataendelea kuwa nazo zikiharibika basi mwisho, wakifariki basi mwisho, hizo ni za kusalimisha kwenye vituo vya polisi.” amesema Millanzi

https://youtu.be/ca-8FXSuZ5g