Hatua zilizochukuliwa na Serikali kuleta ahueni katika bei ya mafuta

0
1618

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwamba, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.

Akiwasilisha taarifa ya Serikali Bungeni, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha 2021/22. Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea.

https://www.youtube.com/watch?v=xUr9Wcs2yJw

Pia waziri Makamba amesema hatua nyingine zisizo za kifedha zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na:

Kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu kufanya hivyo.

Kuanzisha mfuko wa kuhimili ukali wa bei zamafuta (Fuel Price Stabilization Fund).

Kuanzisha hifadhi ya mafuta ya kimkakati (National Strategic Petroleum Reserve).

Kuwa na kituo kikubwa cha mafuta (PetroleumHub).

Kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghalamoja(Single Receiving Terminal – SRT) kupitia maghala ya TIPER ili kupunguza au kuondoa gharama za meli kusubiri au kuchukua muda mrefu katika upakuaji wa mafuta katika maghala mengi.

Kuiongezea uwezo TPDC kuagiza mafuta nje ya nchi, ambapo kwa mara ya mwisho ilifanya shughuli hiyomiaka 20 iliyopita. 21

Kuimarisha utendaji na weledi wa taasisi za Serikali zinazoshughulika na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo EWURA na PBPA (Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja).