Halmashauri sita zapata hati zenye mashaka

0
153

Halmashauri sita kati ya nane zilizopo mkoani Kigoma zimepata hati zenye mashaka kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri ya Mji Kasulu, mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Mji Kasulu, Uvinza, Buhigwe, Kakonko, Kigoma ujiji na Kasulu DC huku halmashauri zilizopata hati ya kuridhisha zikiwa ni Kigoma DC na Kibondo.

Kufuatia taarifa hiyo, Andengenye amezitaka halmashauri zote zilizopata hati zenye mashaka kufanyia kazi hoja zote zilizotolewa na CAG.

Aidha Andengenye ameyaagiza mabaraza ya madiwani mkoani humo kuchukua hatua kwa Watumishi wote watakaobainika kufanya vitendo vya ubadhirifu na kuchangia kuwepo kwa hoja hizo.