Naibu Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka 3.5% mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa mwaka 2022
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.
Aidha Naibu Waziri Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi.
“Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri”Amesema Nderiananga