Hali ya usalama Kipindi cha kampeni shwari

0
202

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini David Misime amesema hali ya usalama na usimamizi wa ulinzi katika kampeni zinazoendelea nchini ni shwari na unaendelea vizuri.

Amesema jeshi la polisi limejiandaa vizuri katika kukabiliana na matishio ya aina yoyote ya kiusalama ambapo ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya nchi ili kuhakikisha kampeni za uchaguzi na uchaguzi mkuu vinafanyika kwa amani na utulivu.

Aidha Kamanda Misime amewatahadharisha wananchi, viongozi wa kisiasa na wadau wengine wa uchaguzi kuendelea kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria za nchi na kutoa onyo kwa wale wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii na yale yote yanayohatarisha uvunjivu wa amani na usalama wa nchi watawajibishwa ipasavyo.