Hakuna Mtanzania anayezuiwa Kutoa maoni ripoti ya CAG

0
417

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa, hakuna Mtanzania anayezuiwa kuijadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwani ni haki yake kikatiba.

Waziri Mwakyembe ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya kuwepo kwa madai ya kuhojiwa na kutishwa kwa baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti uchambuzi wa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, – Zitto Kabwe juu ya uchambuzi wa ripoti hiyo.

Dkt Mwakyembe amefafanua kuwa kilichofanyika ni kuwepo kwa upotoshwaji katika baadhi ya chambuzi hizo na kitendo cha Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas kuwaandikia barua wahusika na kuwaonya kilifanyika kwa mujibu wa sheria.