GGR kusafisha kilo 600 za dhahabu kwa siku

0
133

Serikali imewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kusafisha madini ya dhahabu katika viwanda vya ndani, badala ya kuuza malighafi kwenye viwanda vya nje.

Wito huo umetolewa mkoani Geita na waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko alipotembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR) na kuongeza kuwa, serikali inakosa mapato pamoja na watanzania wanakosa ajira kutokana na malighafii kusafirishwa nje.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa mkoa Geita, Said Nkumba amewataka wafanyabiashara wa madini pamoja na wachimbaji wadogo kupeleka dhahabu yao kusafishwa katika kiwanda cha GGR ili faida ibaki kwa mkoa huo kwa kwa nchi.

Mbunge wa jimbo la Geita, Constantine Kanyasu amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya usafishaji dhahabu ya GGR, Sarah Masasi kwa kujenga kiwanda hicho mkoani Geita na kuongeza kuwa kiwanda hicho ni mkombozi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini.