Gari yagonga treni, mmoja afariki dunia

0
239

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya gari ndogo aina ya Toyota Hilux kugonga treni katika makutano ya reli na barabara eneo la Kilimahewa mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kumkia leo na kusababisha kifo cha dereva wa gari hiyo, Michael Mgombela mwenye umri wa miaka 34.

Kamanda Musilimu amesema, Mgombela maarufu ‘Mwarafu Fighter ‘, ni mwanachama wa chama cha waendesha baiskeli mkoa wa Morogoro na alifariki dunia papo hapo baada ya kutokea ajali hiyo.