Amesema halmashauri zote nchini zimeelekezwa kutenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya programu maalum ya kuwawezesha vijana kushiriki katika kilimo.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo alipokuwa akizindua mpango nufaishi wa kuwawezesha vijana kuingia katika sekta ya kilimo, uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya yanapoendelea maonesho ya wakulima kitaifa maarufu Nanenane.
Amesema fursa zinazotokana na sekta ya kilimo ni nyingi, na hivyo kuwataka vijana kuchangamkia fursa hizo.
Waziri Mkuu amesema mpango huo
nufaishi wa kuwawezesha vijana kuingia katika sekta ya kilimo
aliouzindua hii leo umelenga kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja kuanzia ngazi ya vijana.
Pamoja na hayo amewatoa hofu vijana kuhusu upatikanaji wa mitaji na kusema mikopo ipo kwa maelekezo ya Serikali kwa benki zote nchini kutenga eneo la mikopo kwa ajili ya wakulima na wajasiriamali.