Fountain Gate, TFF, BMT Bungeni

0
190

Baadhi ya viongozi wa michezo nchini, wamefuatana na timu ya shule ya Fountain Gate ya mkoani Dodoma kutembelea Bunge, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakub, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na viongozi kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Shule ya Fountain Gate ilitwaa ubingwa katika mashindano ya Shule Afrika kwa upande wa wasichana, mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa kushirikiana na Motsepe Foundation.

Mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini.